Ukwepaji sheria bado ni changamoto Sudan Kusini-UNMISS

24 Aprili 2017

[caption id="attachment_316197" align="aligncenter" width="616"]sudanwau

Mkurugenzi wa haki za binadamu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS Eugene Nindorera amesema suala la ukwepaji sheria ni moja ya changamoto kubwa nchini humo.

Mkurugenzi huyo hivi karibuni alifanya ziara ya siku tano kwenye eneo la Wau kufuatia machafuko yaliyokatili maisha ya askari 19 na raia 28. Nindorera amesema hakuna mtu aliyekamatwa kwa mauaji hayo yaliyotokea kati ya tarehe 10 na 17 mwezi huu.

Ameongeza kuwa waliokamatwa ofisi yake imebaini kwamba ni wachunga ng’ombe na walikamatwa tu kwa sababu walikuwa na silaha kinyume cha sheria. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba wale waliohusika na mauaji hayo watawajibishwa.

Kwa mujibu wa UNMISS zaidi ya watu 41,000 wanapata hifadhi katika eneo la ulinzi wa raia Wau.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter