Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kibao: Beware! Chaelimisha na kuburudisha

Kibao: Beware! Chaelimisha na kuburudisha

Kwa miaka ishirini ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosaidia kutokomeza mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS imekuwa ikifanya kazi ya kuokoa maisha na kulinda raia dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini. Kazi za UNMAS huendeshwa kwa misingi ya mahitaji ya watu walioathirika na inaendana na hatari za mabomu ya kutegwa ardhini ambazo zinaathiri raia, walinda amani na watoa huduma.

Miongoni mwa mbinu ambazo UNMAS inatumia kuelimisha umma kuhusu hatari za mabomu ya kutegwa ardhini ni kupitia nyimbo, ambapo katika kibao hiki wametumia wimbo, Beware! Ulioimbwa na kundi linalojulikana kama Jay Family wakishirikisha wanafunzi wa shule ya msingi ya wasichana ya Giada huko Sudan Kusini. Basi kwa undani wa kibao hicho ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo.