Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kingono ukomeshwe Sudan Kusini-Owusu

Ukatili wa kingono ukomeshwe Sudan Kusini-Owusu

Ukatili wa kijinsia na kingono ambao huathiri zaidi wanawake na watoto unazidi kuongezeka nchini Sudan Kusini wakati huu ambapo kiwango cha machafuko kimeongezeka, amesema Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Eugene Owusu.

Akizungumza na wanahabari nchini humo hii leo, Bwana Owusu amesema utafiti unonyesha kuwa ukatili wa kingono na kijinsia umeongezeka kwa asilimia 64 mwaka 2016, sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ukwepaji wa sheria.

Amesema hatua hiyo imeongeza hofu kwa wanawake na watoto ambao wengi huhofia kubakwa.

Kiongozi huyo amewaambiwa waandishi wa habri kuwa ukatili dhidi ya wanawake ni kinyume na maadili ya msingi ya binadamau, na kwamba madhila ambayo wanawake na wasichana huyapitia kwa kubakwa ni uasi na unapaswa kukomeshwa.