Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makaburi mapya 17 yagundiliwa DRC-UM

Makaburi mapya 17 yagundiliwa DRC-UM

Makaburi mapya 17 ya pamoja yamegunduliwa katika eneo lililoshuhudia machafuko hivi karibuni baina ya jeshi la serikali na wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umesema Umoja wa Mataifa Jumatano.

(Taarifa ya Amina)

Katika wito wake wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu kisanga hicho, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema wanajeshi wa jeshi la serikali ya DRC waliarifiwa kuhusika baada ya mapigano na wajumbe wa Kamuina Nsapu kwenye jimbo la kati la Kasai mwezi Machi ambapo raia 74 walipoteza maisha.

Ugunduzi huo umekuja wakati DRC iko kwenye hali ya sintofahamu baada ya muhula wa pili wa uongozi wa Rais Joseph Kabila, kumalizika Desemba mwaka jana na uchaguzi kuahirishwa. Liz Throssell ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva.

(Sauti ya Liz)

“Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walizuru Kasai kati ya tarehe 5 na 7 Aprili, ambako waliweza kuthibitisha kuwepo kwa makuburi 17 mengine ya pamoja , na hayo yanafanya idadi ya jumla ya makaburi ya pamoja yaliyothibitishwa kufika 40”