Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzia machafuko lazima kuwe kipaumbele-Guterres

Kuzia machafuko lazima kuwe kipaumbele-Guterres

Kuzuia lazima kuwe kipaumbele kwa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na migogoro na majanga mengine,amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati akizungumza kwenye mkutano wa baraza la usalama ulioangazia haki za binadamu na kuzuia migogoro ya silaha.

Katibu Mkuu amesema kuwa kuzingatia haki za binadamu ni muhimu katika kuimarisha amani na usalama huku akitaja namna juhudi za haki za binadamu kupitia baraza la usalama au operesheni za kulinda amani zimesaidia kulinda raia au kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa uhalifu.

Bwana Guterres amesema kulinda kizazi cha vijana dhidi ya machafuko ni miongoni mwa uwekezaji bora ambao waweza kufanywa na Umoja wa Mataifa katika kutimiza amani endelevu.

( Sauti Guterres)

"Licha ya juhudi zote hizi,mamilioni ya watu bado wanahitaji kulindwa dhidi ya majanga. Zaidi ya yote, muda na rasilimali vinaendelea kutumika kusaidia majanga kuliko kuyazuia . Kama tunataka kukabiliana na changamoto za leo kwa hakika, lazima uzuiaji uwe kipaumbele chetu, kukabiliana na vyanzo vya mgogoro, kusaidia kujenga na kuimarisha taasisi na kuchukua hatua mapema na kwa ufanisi zaidi katika kushughulikia haki za binadamu."

Katibu Mkuu ameongeza kuwa kuimarisha hatua zisizogubikwa na siasa wakati wa kukabiliana na haki za binadmau ni muhimu katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.