Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatutosubiri kutangazwa baa la njaa Somalia kunusuru watoto-UNICEF

Hatutosubiri kutangazwa baa la njaa Somalia kunusuru watoto-UNICEF

Mustakhbali wa maelfu ya watoto nchini Somalia unaendelea kuwa njia panda kutokana na vita, ukame na maradhi kama utapiamlo na kipindupindu.

Kwa mujibu wa Manuel Fontaine mkurugenzi wa operesheni za dharura wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, hawatosubiri baa la njaa kutangazwa nchini humo ili kunusuru maelfu ya watoto hao wanaohitaji msaada wa haraka.

(Sauti ya Fontaine)

“Tunakadiria kwamba tutakuwa na watoto zaidi ya laki mbili watakaokuwa na utapia mlo uliokithiri na idadi itaongezeka, kipindupindu ni tatizo kubwa tuna visa elfu 22 hadi sasa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 700 ukilinganisha na wakati kama huu mwaka jana hivyo hali ni mbaya.”

Ameongeza kuwa ingawa wanaweza kutibu maradhi hayo shida ni fursa ya kuwafikia walengwa nao kufikia huduma.

(Sauti ya Fontaine)

“Tunapeleka timu huko lakini bila shaka fursa itakuwa changamoto kubwa na ulinzi wa watu, na fursa ya watu pia kupata huduma itasalia kubwa suala na changamoto kubwa , hivyo ni kujitahidi kuwa hatua moja mbele badala ya kusubiri kutangazwa kwa baa la njaa, na hivyo ndio tunavyofanya”