Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli za hofu kwenye mikutano ya kampeni Burundi hazistahiki-Zeid

Kauli za hofu kwenye mikutano ya kampeni Burundi hazistahiki-Zeid

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein Jumanne ameelezea kushtushwa na kauli za hofu zilizotapakaa kwenye mikutano ya kampeni katika majimbo mbalimbali nchini Burundi ambapo vijana wa kiumbe kutoka kundi la wanamgambo wa Imbonerakure wakirudia mara kadhaa kuimba wito wa kuwatia mimba au kuwaua wapinzani.

(Taarifa ya Flora)

Kamishna Zeid amesema asili kupangwa kwa maandamano hayo, pamoja na taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea, unaweka  wazi "Kampeni ya hofu" ambayo imekuwa ikiendelea Burundi. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva

(SAUTI YA COLVILLE)

“Video ya kutisha ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii inawaonyesha zaidi ya wajumbe 100 wa Imbonerakure, tawi la vijana la chama tawala CNDD-FDD, wakirudia mara chungu nzima kutoa wito wa wapeni mimba wapinzani ili wazae wana Imbonerakure, na kundi lingine likirudia mara 19 wito wa lazima auwawe”

Ofisi ya haki za binadamu inasema mikutano hiyo imefanyika katika eneo la Ntega, jimbo la Kirundo Kaskazini Mashariki mwa nchi.Kufuatia kutolewa kwa video hiyo Aprili 5 mwaka huu chama tawala CNDD-FDD kimetoa taarifa ya kulaani kauli hizo na kusema uchungu wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ushawishi kutoka nje ya chama .

Hata hivyo  ofisi ya haki za binadamu inasema repoti za karibuni zinaonyesha kwamba mikutano kama hiyo imeandaliwa nchi nzima na maafisa wa serikali na chana cha Rais.