Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambilizi dhidi ya waokoaji Syria

UM walaani mashambilizi dhidi ya waokoaji Syria

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi dhidi ya waokoaji 5000 nchini Syria katika eneo la Magharibi mwa Allepo yaliyoripotiwa leo.

Waokoaji hao walikuwa wanasafiri kutoka miji ifahamikao kama Foah na Kefraya kulelekea maeneo yanayokaliwa na serikali

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo imemnukuu kingozi huyo António  Guterres akituma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia majeruhi upionyaji wa haraka.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uokozi ulikuwa unafanyika kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya miji mine.

Bwana Guterres amezitolea wito pande kinzani kuhakikisha usalama kwa wanaosubiri kuokolewa na kuongeza kuwa waliohusika na shambulio la leo wanapaswa kufikishwa katika mkono wa sheria.