Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi watatu wa WFP wauawa Sudan Kusini: WFP

Wafanyakazi watatu wa WFP wauawa Sudan Kusini: WFP

Mabawabu watatu raia wa Suda Kusini ambao walikuwa wanafanya kazi na  shirika  la mpango wa chakula duniani WFP wameuawa jumatatu  juma hili  wakati  wakielekea kazini mjini Wau.

Taarifa ya WFP iliyotolewa jumatatu imesema kuwa wawili kati ya wanaume hao wamekufa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga ilihali mmoja aliuawa kwa kufyatuliwa risasi.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS,  uliripoti mapema juma hili kuwa watu 16 waliuawa mjini Wau Jumatatu baada ya vikosi vya serikali kushambulia mji huo.

WFP imesema kuwa mnamo Alhamisi ilibaini kuwa wahandisi wake watatu walikuwa miongoni mwa waliouawa.

Mkuu wa shirika hilo la mpango wa chakula nchini Suda Kusini Joyce Luma amesema WFP imesononeshwa na vifo vya wafanyakazi hao ambao walifanya kazi kila siku ili kuwapatia chakula cha uokozi raia wenzao.

Kwa mujibu wa shirika hilo waliouawa ni  Daniel James, Ecsa Tearp and Ali Elario.