Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malaria janga Burundi,UM wakabiliana nalo-Mbilinyi

Malaria janga Burundi,UM wakabiliana nalo-Mbilinyi

Nchini Burundi, licha ya changamoto za kiafya ikiwamo uwepo wa ugonjwa wa malaria, na mahitaji ya chakula, hali ya mahitaji ya kibinadamu nchini humo imeimarika katika taifa hilo ambalo limekumbwa na mzozo wa kisiasa.

Akizungumzia tathimini ya kipindi cha robo tatu ya mwaka 2017, Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Abel Mbilinyi, ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa ugonjwa wa malaria ambao ulitangazwa na serikali ya Burundi kuwa ni janga, unakabiliwa kwa ushirikianao wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

(Sauti Mbilinyi)

Kuhusu ukame uliosababisha ukosefu wa chakula, Mbilinyi anasema kile ambacho Umoja wa Mataifa unakifanya.

(Sauti Mbilinyi)