Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stuka! Sonona chanzo cha ulemavu, inatibika: WHO

Stuka! Sonona chanzo cha ulemavu, inatibika: WHO

Sonona hutokana na athari za kisaikolojia, miongoni mwa vichochezi ni migongano baina ya watu, familia au jamii, pamoja na kushindwa kutimiza  au kutimiziwa malengo kadhaa.

WHO inasema ugonjwa huo sasa ni tishio na haupewi kipaumbele duniani. Zaidi ya watu milioni 300 wanakabiliwa na sonona.

Tuzungumze ndiyo kauli mbiu inayotumiwa  katika kupazia sauti elimu dhidi ya sonona, ikitaka mtu kueleza wazazi,walezi, wataalamu wa afya au hata marafiki juu ya mambo yanayomsibu,kwa kuwa inasaidia kuepuka upweke na kuleta nafuu hata uponyaji.

Shirika la afya ulimwenguni limeandaa kampeni mbalimbali za elimu kwa umma. Mwenzangu Selina Cherobon ameingazia video mojawapo katika wavuti wa WHO tuungane naye.