Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapitisha azimio la kuanzisha ujumbe mpya Haiti

Baraza la usalama lapitisha azimio la kuanzisha ujumbe mpya Haiti

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo Alahmisi limepitisha kwa kauli moja azimio la kufunga ujumbe wa umoja huo nchini Haiti MINUSTAH, hatau inayopisha ujumbe mpya mdogo nchini humo.

Ujumbe wa usaidizi wa haki nchini Haiti utakaofahamika kwa kifupi MINUJUSTH, utaanza majukumu yake Oktoba 15, ukiwa na mamlaka ya kusaidia serikali kuimarisha utawala wa sheria,sera na ulinzi wa haki za binadamu.

Baraza hilo katika kikao cha leo limetabua hatua zilizofikiwa na Haiti baa da ya mchakato wa uchaguzi miezi michache iliyopita, ambapo Rais na Waziri Mkuu mpya wameingia madarakani.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Umooja wa Mataifa, kikosi cha ulinzi wa amani cha MINUSTAH kitasalia nchini humo na kuondoka tararibu kwa kipindi cha miezi sita ijayo, wakati ujumbe utasalia ili kuwezesha MINUJUSTH, ambayo itaimarisha kikosi cha polisi kilichoundwa , kwa kipindi cha miezi sita.

Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa Balozi Nikki Haley, amesema ujumbe unaosalia utaendeleza wajibu wa ulinzi kwa raia na kwamba.

( Sauti Nikki Haley)

‘‘Uwajibikaji na kutoa taarifa kumeongezwa ili tuweze kufuatilia ufanisi wa watumishi wanaosalia. Vituo viwili vitaondolewa ili kuongeza nguvu katika maeneo yanayohitaji zaidi msaada. Ujumbe wa utulivu unapoondoka na ule mpya ukiwasili, watu wa Haiti watahakikishiwa uhuru na kujitegemea.’’