Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda, Kenya, Tanzania na DRC vyachukua hatua kutokomeza ADF

Uganda, Kenya, Tanzania na DRC vyachukua hatua kutokomeza ADF

Uwepo wa vikundi haramu vilivyojihami huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC umeendelea kuwa tishio kwa amani na usalama nchini humo na ukanda mzima wa Maziwa Makuu.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo Said Djinnit amesema hayo alipohutubia Baraza la Usalama la umoja huo,ambalo lilikutana mahsusi kujadili utekelezaji wa mkataba wa amani, usalama na ushirikiano kwa DRC na ukanda wa Maziwa Makuu, mkataba uliotiwa saini miaka minne iliyopita.

Ametaka juhudi ziendelee kutokomeza vikundi hivyo ambavyo ni pamoja na kile cha FDLR na ADF, akiunga mkono kinachoendelea kufanyika kwa ushirikiano kati ya jeshi la serikali na lile la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO huku akisema..

(Sauti ya Djinnit)

“Nakaribisha uzinduzi wa tarehe 18 mwezi Februari mwaka huu uliofanywa na DRC, Kenya, Uganda na Tanzania wa mfumo wa pamoja wa ufuatiliaji utakaoshughulikia ongezeko la kitisho cha ADF. Natoa wito kwa nchi husika kuchangia ipasavyo kwa mfumo huo ili upatiwe rasilimali za kutosha kutekeleza lengo lake.”