Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumaini ni wimbo wa kusongesha maisha kwa wahanga wa mauaji Rwanda

Matumaini ni wimbo wa kusongesha maisha kwa wahanga wa mauaji Rwanda

Miaka 23 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, kumbukizi zinaendelea kufanyika huku watoto ambao waliachwa na wazazi wao, sasa wakiwa wamekuwa wakubwa na kukumbuka maisha wakati wa uhai wa wazazi wao. Uhusiano wa kifamilia wakati huo umesalia kumbukumbu nzuri kwa watoto hao, simulizi ambazo mmoja wao alitoa wakati wa tukio la kumbukumbu la mauaji ya Rwanda lilikofanyika jijini New York, Marekani kwa uratibu wa taasisi ya kusaidia wahanga, GSSN. Je nini kilifanyika? Assumpta Massoi alikuwa shuhuda wetu.