Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Samaki haramu kutowafikia walaji-FAO

Samaki haramu kutowafikia walaji-FAO

Juhudi za shirika la kilimo na chakula FAO kuhakikisha uwepo wa viwango vya kimataifa vya kuongoza kuzuia samaki waliopatikana kwa njia ovu kutomfikia mlaji zimepiga hatua kwa kupitishwa rasimu ya muongozo huo.

Taarifa ya FAO imeeleza kwamba hatua hiyo imefikiwa juma lililopita baada ya kupitishwa bila kupingwa kwa waraka huo wakati wa mashauriano ya kiufundi yaliyomaliza miaka mitano ya juhudi hizo.

Waraka wa rasimu hiyo unatarajiwa kuwasilishwa kwa nchi wanachama wa FAO kwa ajili ya kupitishwa wakati wa mkutano mjini Rome Italia mnamo Julai tatu hadi nane mwaka huu.

Ikiwa rasimu ya muongozo huo itapitishwa na serikali, shirika hilo la kilimo na chakula limesema utakuwa ni viwango bora vya kuwezesha wafanyabiashara na mataifa kuanzisha mfumo wa kudhibiti samakai kuanzia kwenye kuvuliwa hadi kwenye sahani ya mlaji