Masahibu ya ukame Somalia ni zaidi ya njaa

Masahibu ya ukame Somalia ni zaidi ya njaa

Machungu ya ukame nchini Somalia yameendelea kukumba wananchi hususan wale ambao wamekumbwa na magonjwa yatokanayo na ukame. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Katika moja ya hospitali ya mji wa Baidoa kwenye jimbo la Kusini-Magharibi nchini Somalia, Habiba Ahmed akiuguza mama yake mzazi ambaye anaugua kutapika na kipundupindu, moja ya magonjwa yasababishwayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Habiba ameueleza ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioongozwa na mkurugenzi wa operesheni wa ofisi ya usaidizi wa kibinadamu OCHA, John Ging kuwa mama yake anapata nafuu sasa.

Huko Kismayo, jimbo la Juba Kusini, walitembelea mama ambaye aliambukizwa kipindupindu wakati akimhudumia mwanae..

Na ndipo Bwana Ging akasema walichokubaliana na mamlaka za majimbo hayo mawili..

Tumezungumza jinsi ya kushirikiana ili kukabili ukame na kuepusha njaa, ili watu waweze kupata msaada wanaohitaji.”