Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi, wahamiaji wenye ulemavu wapewe kipaumbele-Wataalamu

Wakimbizi, wahamiaji wenye ulemavu wapewe kipaumbele-Wataalamu

Rasilimali fedha, na watu waliojitoa wanahitajika kwa ajili ya kundi la watu wenye ulemavu katika mkakati wa kimataifa wa wakimbizi na wahamiaji wamesema wataalamu wa Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi mashauriano na serikali.

Mkakati huo wenye maudhui ya usalama na mpangilio kwa wakimbizi unatarajiwa kuzinduliwa mwaka 2018, utaweka kanuni na maazimio baina ya serikali ili kuanzisha uratibu kwa uhamiaji wa kimataifa.

Katika taarifa yao ya pamoja kuhusu kujumuisha watu wenye ulemavu wataalamu hao mathalani Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu ulinzi wa haki za wafanyakazi wahamiaji na familia zao, Jose Brillantes, amesema ni muhimu viongozi kote duniani kuweka ahadi ya uokozi wa maisha ya wakimbizi na wahamiaji, kulinda haki zao bila kusahau wale wenye ulemavu.

Naye mtaalamu maalum wa haki za watu wenye ulemavu Catalina Devandas Aguilar, amesema nchi nyingi hazina utaratibu maalum wa kuwatambua wakimbizi na wahamiaji wenye ulemavu hivyo kushindwa kuwapa huduma muhimu kama vile malazi na huduma za afya mujarabu kwa hali zao.