Skip to main content

Mchango wa EU kuimarisha afya kwa wanawake na wasichana Iraq-UNFPA

Mchango wa EU kuimarisha afya kwa wanawake na wasichana Iraq-UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la idaidi ya watu UNFPA linasema mchango wa kiasi cha Euro milioni tano kutoka jumuiya ya Ulaya utawezesha shirika hilo, kuongeza msaada wa dharura wa huduma za afya kwa wanawake na wasichana katika migogoro nchini Iraq.

UNFPA inasema kiasi hicho cha fedha ambacho ni sawa na dola za Kimarekani milioni 5.3 pamoja na mambo mengine, kitatumiwa katika huduma za uokozi za afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana waliofurushwa huko Mashariki na Magharibi mwa Mosul.

Jeshi la Iraq na washirika wake, hivi karibuni wamekomboa maeneo hayo yaliyokuwa chini ya ngome ya kundi lenye msimamo mkali ISIL au Daesh.

UNFPA kadhalika imesema mchango wa EU unasaidia manunuzi na uendeshaji wa vituo viwili, kimoja cha ugawaji misaada na kituo cha afya ya uzazi kitembeacho, katika kuzifikia wilaya za maeneo hayo pamoja na majimbo mengine matatu ya Iraq.