Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya kemikali yastitajwe tena duniani-Feltman

Matumizi ya kemikali yastitajwe tena duniani-Feltman

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana katika mkutano wa dharura leo kujadili kuzorota kwa amani nchini Syria siku mbili baada ya madai ya shambulizi mjini Khan Sykun jimboni Idlib, linalodaiwa kuwa la kemikali lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 100 wengi wao wakiwa watoto na zaidi ya 70 kujeruhiwa.

Mkutano wa baraza hilo umefanyika muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kulaani mashambulizi yanayozorotesha amani nchini Syria huku akiinyoshea kidole Marekani kwa kitendo chake cha hapo jana cha mashambulizi ya anga dhidi ya kituo cha kijeshi cha Shayrat.

Akizungumza katika mkutano wa baraza la usalama hii leo, Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amesisitiza kuwa umoja huo na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhakikisha matumizi ya kemikali hayatajwi tena.

Amesema hayo yote yanaikumbusha dunia kwamba suluhisho la mgogoro wa Syria kamwe sio la kijeshi bali ni la kisiasa na kwamba.

( Sauti Feltman)

‘‘Ulinzi wa raia na uwajibishwaji unapaswa kuwa kipauambele cha ajenda yetu ya amani. Nchini Syria, ulinzi huo hauwezekani ikiwa pande kinzani, serikali na upinzani wataruhusiwa kutekeleza mambo na kukwepa sheria, na kama serikali ya Syria itaendelea na uvunjifu wa haki za binadamu kwa raia wake .’’