Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji wa uhalifu uzingatie sheria za kimataifa na maazimio ya baraza la usalama-UM

Uwajibikaji wa uhalifu uzingatie sheria za kimataifa na maazimio ya baraza la usalama-UM

Kuna haja ya uwajibikaji wa uhalifu kama wa Khan Shykun Syria lakini uwajibikaji huo lazima uzingatie sheria zilizopo za kimataifa na maazimio ya baraza la usalama. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Kauli hiyo imetolewa Ijumaa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema amekuwa anafuatilia kwa karibu hali inayoendelea Syria na amepata taarifa za mashambulizi ya anga dhidi ya kituo cha kijeshi cha Shayrat Syria yaliyotekelezwa na Marekani.

Kupitia taarifa ya msemaji wake Guterres ametoa wito wa kujizuia na vitendo vyovyote vitakavyozidisha madhila kwa watu wa Syria.

Ameongeza kuwa baraza la usalama lina wajibu kwa ajili ya amani na usalama wa kimataifa na amelitolewa wito wa kuungana na kutekeleza wajibu wao.