Operesheni za ulinzi wa amani ziko njia panda, tushikamane:Guterres

6 Aprili 2017

Operesheni za amani ziko njia panda na jukumu la Umoja wa Mataifa ni kuziwekea mikakati sahihi iliyo wazi, inayowezekana na msaada. Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye mjadala wa baraza la usalama Alhamisi kuhusu tathimini ya operesheni za ulinzi wa Amani. Ameongeza kuwa mafanikio ya operesheni hizo yanategemea juhudi za kila mmoja.

(GUTERRES CUT 1)

Ulinzi wa Amani wa Umoja wa mataifa ni uwekezaji katika Amani ya kimataifa, usalama na mafanikio na mafanikio ya shughuli za amani ni chanzo cha fahari kubwa kwetu sote, wanaposhindwa hutuumiza na kusukuma kuziboresha”

Ameongeza kuwa mikakati madhubuti inahitajika ambayo itasaidia operesheni hizo kuanzia kuzuia , kutatua migogoro , kulinda amani , ujenzi wa amani na mipango ya muda mrefu ya maendeleo na kwamba operesheni za amani zinatofautiana na mafanikio yake ni lazima wadau wote watimize wajibu wao zikiwepo serikali.

Amesema kwa ajili ya mustakhbali wa muda mrefu kuna mambo tisa ya kufanyia mabadiliko

(GUTERRES CUT 2)

“Mosi nimeunda timu ya kutathimini jinsi gani ya kuboresha mchakato wa amani na usalama na wataripoti kwangu Juni, pili tunahitaji utendaji na uwajibikaji, tatu operesheni za amani zinahitaji majukumu yaliyo wazi yanayowezekana na yanayokwenda na wakati kutoka kwa baraza hili, nne wanawake lazima wawe na jukumu kubwa katika operesheni za amani kama askari, polisi na wafanyakazi raia."

image
Mlinda amani wa senegal kutoka mpango wa UM wa MINUSMA Mali akizungumza na raia wa Mali wakati wakishika doria nje ya uwanja wa Mamadou Konate wakati wa tukio la kuchagiza amani. Picha na UM//Marco Dormino

Ameongeza kuwa mambo mengine ni(GUTERRES CUT 3)

"Tano tunahitaji mkakati bora na uliopangwa vizuri, udhibiti na uongozi wa operesheni zetu na mkakati. Sita lazima tuongeze matumizi ya teknolojia ya kisasa, saba tunahitaji kuwasiliana na kuengeza uelewa kwamba operesheni za amani za Umoja wa Mataifa ni lazima kwa amani ya dunia , usalama na mafanikio, nane tunahitaji kuimarisha muhusiano na washirika wetu wa kikanda na kimaeneo na tisa na miwsho ushirika huo lazima uwe katika msingi imara , na ufadhili unaotabirika.

Guterres amesema anategemea umoja na mshikamano wa baraza la usalama ili kutekeleza wajibu wa kuhakikisha amanai na uslama wa kimataifa katika dunia hii inayobadilika.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter