Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahandisi wa UNMISS wafungua duka la vitamtamu na mbogamboga Bor

Wahandisi wa UNMISS wafungua duka la vitamtamu na mbogamboga Bor

Wahandisi wa kikosi cha Korea Kusini kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wamefungua duka la vitamutamu na mboga mjini Bor kama sehemu ya kituo cha mafunzo ya kiufundi.

Duka hilo Habit Market lililofunguliwa Alhamisi ni mradi wa juhudi za kikosi hicho kuwawezeshwa wanafunzi kwa kuwapa mafunzo ya ujuzi wa biashara na mahusiano ya wateja.

Hanbit Market itawapa fursa wanafunzi kuuza mbogamboga na masomo ya kuoka vitu bekari, huku wakati huohuo wakichangia maendeleo ya uchumi kwa wakulima na jamii za eneo hilo.

Katika uzinduzi wa duka hilo kamanda wa kikosi hicho cha Korea Kusini kanali Deuk-Sang Ahn amesema Hanbit Marketitawasaidia sana pia wafanyakazi wa UNMISS kwandi ndio hasa walengwa na faida haitopotea kwani itarejea tena kwa wanafunzi na kuboresha mafunzo na wanafunzi watakuwa wamenufaika na ujuzi endelevu wa biashara.