Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuenzi wahanga wa mauaji ya kimbari Rwanda kwa kuchukua hatua- Guterres

Tuenzi wahanga wa mauaji ya kimbari Rwanda kwa kuchukua hatua- Guterres

Leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya mauaji yakimbari nchini Rwanda yaliyotokea miaka 23 iliyopita, Umoja wa Mataifa ukisema kuwa kitendo cha maridhiano kutoka kwa waathirika sambamba na uwezo wao wa kuibuka upya na kuendelea na maisha ni jambo la hamasa kwa kila mtu duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake amesema ni kwa mantiki hiyo kuwa njia pekee ya kuheshimua waathirika na pia kuenzi zaidi ya watu 800,000 waliokuwa wakiwemo watutsi na wahutu wenye msimamo wa kati ni kuhakikisha halijirudii tena.

Amesema dunia inapaswa kuwa makini na kusoma alama za maonyo dhidi ya matukio ya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua kuyatokomeza kwa kuwa ..

(Sauti ya Guterres)

“Hata hii leo, makundi madogo na mengineyo yanashambuliwa na kunyanyaswa kwa jinsi walivyo. Hebu na tujifunze na kile kilichotokea Rwana na pamoja tufanye kazi kujenga mustakhbali wa utu, stahmala na haki za binadamu kwa wote.”