Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yawafunda wanafunzi Sudan Kusini

UNMISS yawafunda wanafunzi Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha semina kwa wanafunzi zaidi ya 100 wa chuo kikuu cha Bahr el-Ghazal huko Wau na kuwafunza kuhusu majukumu, mamlaka pamoja na changamoto zainazokabili ujumbe huo.

Kaimu Mkuu wa chuo hicho Profesa Samson Wasara amesema semina hiyo imekuja kwa wakati muafaka kwani wanafunzi wa chuo hicho wanawezeshwa pia kufahamu masuala mbalimbali kuhusu nchi yao hivyo mafunzo yamewapa mtizamo sahihi kuhusu majukumu ya UNMISS.

Amesema hiyo ni sehemu ya shughuli za ziada sio tu kwa chuo bali pia kwa taifa na kuongeza kuwa semina hiyo izingatiwe kama swehemu ya eleimu ya uraia nchini Sudan Kusini.

Kwa upande wake mkuu wa mashinani wa UNMISS Winnie Babihuga, amesema kwa kujihusisha na wadau kadhaa wa taifa hilo na kupokea maoni yao moja kwa moja ni muhimu kwa kutambua maeneo ambayo ujumbe huo waweza kufanya kazi kwa karibu na jamii.

Amewataka wanafunzi nchini humo kutumia uadilifu wao na kujielekeza katika kupigia chepuo amani.