Skip to main content

WHO yahaha kusheheni dawa kutibu wahanga wa Idlib

WHO yahaha kusheheni dawa kutibu wahanga wa Idlib

Shirika la afya ulimwenguni WHO, linaendelea kusheheni vifaa vya matibabu zikiwemo dawa ili kusaidia wahanga wa shambulio lililofanyika jana huko Khan Shaykun jimbo la Idlib nchini Syria, ambalo linadaiwa kuwa ni la silaha za kemikali.

Msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema kuwa wanapeleka vifaa hivyo huko Uturuki ambako kuna ofisi yao na pia maeneo ya Idlib nchini Syria kwa kuwa..

(Sauti ya Tarik)

Kila mtu ambaye aliona picha za jana hawezi kuwa na mtazamo tofauti juu ya machungu wanayopata wananchi wa Syria.”

Hata hivyo amesema katika shambulio hilo lililosababisha vifo vya watu 70 na mamia kadhaa wamejeruhiwa...

(Sauti ya Tarik)

“WHO haiwezi kuthibitisha kuwa ni kweli kemikali ilitumika, nani alitumia au ni aina gani ya kemikali ilitumika.”

Amesema jukumu hilo la kuchunguza na kubaini nini kilitumika au nani alitumia ni la shirika linalopinga matumzi ya silaha hizo OPCW.