ILO yaendesha mjadala wa mustakabali wa kazi

5 Aprili 2017

Mjadala wa siku mbili kuhusu mustakabali tunaoutaka kwa kuzingatia muktadha wa kazi utaanza kesho mjini Geneva Uswisi, limesema shirika la kazi duniani ILO kupitia wavuti wake.

Kwa mujibu wa ILO, mabadiliko yanayoshuhudiwa ulimwenguni hivi sasa yanatoa changamoto kuwaza mustakabali wa ajira ili kukabiliana na mageuzi katika mwelekeo haki ya kijamii.

Mjadala huo utakaorushwa mbashara na wavuti huo utahusisha wadau kadhaa wa masuala ya ajira kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambapo mada kama vile kazi za heshima kwa wote, mitizamo ya vijana kuhusu kazi, mpangilio wa kazi na uzalishaji pamoja na utawala wa kazi zitajadiliwa.

Mwaka 2013, ILO iizindua jukwaa la mustakabali wa kazi ambalo pamoja na mambo mengine lina jukumu la kuratibu mijadala kama huo unaoanza hapo kesho April tano.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter