Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimesikitishwa na shambulio la silaha za kemikali Syria

Nimesikitishwa na shambulio la silaha za kemikali Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres amesema amesikitishwa na taarifa za madai ya matumizi ya silaha za kemikali katika shambulio la anga kwenye eneo la Khan Shaykhun kusini mwa jimbo la Idlib, Syria na ametuma salamu za rambirambi za dhati kwa waathirika wa tukio hilo na familia zao .

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Umoja wa mataifa hivi sasa hauko katika nafasi ya kuthibitisha taarifa hizo.

Ujumbe wa kutafuta ukweli kuhusu matumizi ya silaha za kemikali wa shirika linalopinga matumzi ya silaha hizo OPCW umetangaza kwamba umeanza kukusanya taarifa ili kujaribu kuthibitisha matumizi ya silaha hizo.

Guterres amekumbusha kwamba baraza la usalama siku za nyuma liliweka bayana kuwa matumizi yoyote ya silaha za kemikali popote ni tishio la amani na usalama wa kimataifa na kwamba matumizi ya silaha za kemikali ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.