Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kwa ajili ya Syria ukianza , UM waonya dhidi ya ukataji ufadhili

Mkutano kwa ajili ya Syria ukianza , UM waonya dhidi ya ukataji ufadhili

Wakati mkutano mkubwa wa kimataifa umeanza leo mjini Brussels Ubelgiji, mashirika ya Umoja wa mataifa yameonya kwamba kudorodra kwa msaada wa fedha kutoka nchi wanachama kutauweka njia panda msaada muhimu kwa mamilioni ya wakimbizi wa Syria na jamii zinazowahifadhi.

image
Mratibu wa Umoja wa mAtaifa wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura (OCHA) Stephen O’Brien. Picha: UM
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mratibu wa Umoja wa mAtaifa wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura (OCHA) Stephen O’Brien amesema ikiwa ni zaidi ya miaka sita tangu kuzuka mzozo wa Syria, ukatili, mauaji, uasi na jinamizi la hali ya juu vimeighubika Syria na kama wahudumu wa kibinadamu “tumepita wakati wa kutoa tahadhari bali ni wakati wa kushikamana na wahitaji, kwa wakati wote ambao vita vitaendelea , ni lazima kuwa tayari na rasilimali za kutosha kukabiliana na mahitaji, ulinzi na kufikisha msaada kwa watu wa Syria.

Ameongeza kuwa dunia bado ina fursa ya kuonyesha mshimakano na watu walio katika madhila, kuwasaidia , binafsi, bila ubaguzi, kisiasa, na bila masharti yoyote ili kuokoa maisha yao popote walipo, kwa njia yoyote na wakato wowote.

image
Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)
Kwa upande wake Kamishina mkuu wa wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi amesema hali inazidi kubwa mbaya, Syria ikisalia kuwa moja ya mgogoro mkubwa kabisa wa kibinadamu. Na ombi la msaada kwa ajili ya Syria lililozinduliwa Januari mwaka 2017 likihitaji dola bilioni 4.63 kwa ajili ya wakimbizi na jamii zinazowahitaji , leo hii ni dola milioni 433 tu au asilimi 9 ya fedha zinazohitajika ndio zilizopatikana.

Amesema wanawashukuru wote waliojitolea hadi sasa lakini ukweli ni kwamba ufadhili hauendi sanjari na mahitaji, na watu milioni 13.5 wanaume, wanawake na watoto ndani ya Syria wanahitaji msaada wa haraka. Watu wengine zaidi ya milioni 5 ni wakimbizi nchi jirani za Misri, Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki ,huku wengine kwa maelfu wamefanya safari za hatari kwenda Ulaya na kwingineko kukimbia vita.

image
Mkuu wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Helen Clark.(Picha:UM/Rick Barjonas)
Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP Helen Clark amesema bila ongezeko la ufadhili maeneo yote ya msaada yataathirika.

Chakula na msada wa fedha taslimu vitapunguzwa au kukatwa kabisa katikati ya mwaka huu na kuongeza changamoto za utulivu na usalama katika ukanda mzima.

Ameongeza kuwa hadithi katika eneo zima ni ilele huduma za maji na usafi, ajira na soko la nyumba vyote viko katika hatihati.

Amesema inganwa UNDP na wadau wako huko kusaidia masuala ya miundombinu, kuboresha maisha ya watu na kuleta maendeleo katika jamii lakini mahitaji ni makubwa na msaada unahitajika haraka.

Mkutano huo utaendelea Jumatano ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kuhutubia.