Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya kudumu ndio muarobaini wa ukame Somaliland

Suluhu ya kudumu ndio muarobaini wa ukame Somaliland

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amekamilisha ziara ya siku mbili Somaliland kutathmini jinsi zahma ya ukame inavyoathiri watu nchini humo kwa muda sasa na kuangazia hali halisi iliyvo kwa jumuiya ya kimataifa . Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Katika ziara hiyo amekutana na Rais Ahmed Mohamoud Silanyo, mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na wazee wa vijiji, hususan kujadili jinsi ya kuongeza na kuboresha usaidizi, na kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu kwa wakazi wa Somaliland, waliohatarini kupatwa na ukame mwingine katika siku za karibuni.

Keating ametembelea kijiji cha Laaca ambacho ni mwenyeji wa waathirika, na amesema kimelemewa na hakina hata rasilimali za kukidhi mahitaji yao wenyewe. Amejionea jamii zenye kupambana na changamoto ya ukosefu wa lishe na makazi bora, na kusema zimo hatarini zaidi pindi msimu wa Gu wenye mvua kali na mafuriko unaoletaleta magonjwa kama vile kipindupindu.

Ameshukuru wadau wa kimataifa kwa usaidizi wao, na ametoa wito wa kuongeza maradufu msaada wao na kuzingatia ni jinsi gani inaweza kujenga uwezo wa watu hawa kukabiliana na tatizo hili la mara kwa mara.

Mkuu wa @UNSomalia @SRSGKeating atembelea #Somaliland kutathmini hali ya ukame na usaidizi pic.twitter.com/u8dmUx8lWf

— UN News Kiswahili (@UNNewsKiswahili)
April 4, 2017