Asilimia 100 ya nishati mbadala 2050 inawezekana-UNEP
Ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu inaonyesha kwamba wataalamu wengi wa nishati mbadala wanakubali kwamba kuwa na asilimia 100 ya nishati mbadala katika kiwango cha kimataifa ifikapo 2050 “inawezekana na ni yakinifu” limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP.
Ripoti hiyo "Hatima ya nishati duniani:mdahalo kuelekea asilimia 100 ya nishati mbadala” iliyotolewa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa New York na REN21 mtandao wa wadau mbalimbali inachambua mitazamo ya wataalamu 114 wa nishati mbadala kutoka katika kila kanda duniani waliohojiwa mwaka 2016.
Sven teske kutoka chuo kikuu cha teknolojia Sydney na mwandishi wa ripoti hiyo amesema asilimia 71 ya wataalamu ama wanakubali au kukabiliana kabisa na kauli hiyo wakati asilimi 29 ama hawaafiki au kutokubaliana kabisa.
Naye mkurugenzi mtendaji wa REN21 Christine Lins amesema
(Sauti ya Christine)
“Mwaka 2016 umekuwa mwaka wa tatu mfululizo ambapo uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa asilimia 3, lakini uchafuzi wa hewa utokanao na sekta ya nishati umepungua”
Ameongeza kuwa sababu kubwa ni uwekezaji katika nishati mbadala hasa Uchina na Marekani na hivyo nishati hiyo..
(Sauti ya Christine)
"Kwa upande mmoja inaingia kwenye mifumo ya nishati katika nchi nyingi, lakini pia tunaona kwamba tumetoka mbali. Tuna asilimia 20 ya matumizi ya nishati duniani siku hizi yanayotoka katika nsihati mbadala”
Kwa mujibu wa ripoti, inakadiriwa kuwa watu milioni 100 hivi sasa wanapata nishati ya umeme kupitia mifumo iliyosambazwa ya nishati mbadala na masoko ya mifumo hiyo yanakuwa kwa kasi.