Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani shambulizi la St. Petersburg

Guterres alaani shambulizi la St. Petersburg

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulizi la bomu lililokatili maisha na kujeruhi wengi hii leo katika mji wa St. Petersburg, Urusi.

Kwa kupitia msemaji wake Stephane Dujarric, ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Urusi na amesema wahusika wa tukio hilo ni lazima wawajibishwe.