Miili ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu kutoka Kenya waliouawa Sudan Kusini kusafirishwa

31 Machi 2017

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed Ijumaa ametangaza kwamba miili ya wahudumu wa misaada watatu kutoka Kenya waliouawa mwishoni wa wiki iliyopita nchini Sudan kusini itasafirishwa kesho Jumamosi kutoka Juba na kurejeshwa nyumbani Kenya.

Ubalozi wa Kenya Juba na ubalozi wa Sudan Kusini Nairobi wanashirikiana kuratibu zoezi hilo.

Wahudumu hao ni miongoni mwa wahudumu sita wa misaada ya kibinadamu waliouwa wakisafiri kutoka Juba kuelekea Pibor Jumamosi iliyopita.

Walikuwa wakifanya kazi na shirika lisilo la kiserikali la uwezeshaji na maendeleo mashinani CREDO linalofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter