Uamuzi wa Israel kuhusu makazi mapya ya walowezi umenisikitisha-Guterres

31 Machi 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa na kutiwa shaka na uamuzi wa Israel wa kujenga makazi mpaya ya Walowezi kwenye eneo linalokaliwa la Wapalestina.

Kupitia ujumbe uliotolewa na msemaji wake Ijumaa, Katibu Mkuu amekuwa akisisitiza kila wakati kwamba hakuna mpango mbadala kwa Waisrael na Wapalestina kuishi pamoja kwa mani na usalama.

Na amelaani hatua zote kama hii ya sasa ambayo inatishia mustakhbali wa amani na suluhu ya kuwa na mataifa mawili.

Ameongeza kwamba makazi hayo ni haramu chini ya sheria za kimataifa na ni kikwazo kwa mchakato wa amani.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter