Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshikamano wahitajika zaidi hivi sasa kusaidia raia huko Mosul- Guterres

Mshikamano wahitajika zaidi hivi sasa kusaidia raia huko Mosul- Guterres

Akiwa bado Mashariki ya Kati kwa ziara katika ukanda huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametembelea kambi ya wakimbizi ya Hassan Sham, kaskazini mwa Iraq.

Guterres amepata fursa ya kuzungumza na wakimbizi wa ndani pamoja na watu wa kabila la Yazid, wakati huu ambapo mapigano ya kukomboa mji wa Mosul yameingia mwezi wa saba.

Baada ya ziara hiyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa raia wamekumbwa na machungu na bado machungu yanaendelea chini ya ukandamizaji wa magaidi wa ISIS.

Hivyo amesema wakati wa operesheni za kutokomeza ugaidi wa ISIS jambo muhimu ni mshikamano..

(Sauti ya Guterres)

“Mshikamano na wale wanaokomboa Mosul. Mshikamano na raia wanaopata machungu. Ushirikiano ili kuwahakikishia ulinzi raia na wakati huo huo mshikamano na wahanga na kuweka mazingira bora ya maridhiano. Kila kitu kinahitaji uwigo mpana wa ahadi kutoka jamii ya kimataifa. ”