Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yaunda kikosi cha kuboresha miji.

ITU yaunda kikosi cha kuboresha miji.

Shirika la Umoja wa Mataifa la teknolojia ya taarifa na mawasiliano ITU limeunda kikosi lengo kwa ajili ya kutafiti uchakatuaji wa taarifa na usimamizi katika muktadha wa miji erevu, ili kufikia kiwango cha ITU.

Taarifa ya ITU inasema kwamba kundi hilo li wazi katika ushirikiano na kundi lolote linalohitaji kufanya hivyo ili kufanikisha ujumuishwaji wa teknolojia ya taarifa na mawasiliano (ICTs) katika mifumo ya miji na kuweka ramani za miji duniani.

Kundi hilo linatarajiwa kutumia teknolojia hiyo kukuza uelewa kuhusu miji tata na mazingira na namna usimamizi wa taarifa fanisi unavyoweza kutoa nuru kwa sekta binafsi na za umma katika ugunduzi unaowezesha ukuajii wa mazingira endelevu katika miji.

Kwa mujibu wa ITU Mwenyekiti wa kundi hilo ni Gyu Myoung Lee wa chuo cha sayansi na tekenolojia cha nchini Korea Kusini.