Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziara yangu Iraq ni kuonyesha mshikamano:Guterres

Ziara yangu Iraq ni kuonyesha mshikamano:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema yuko nchini Iraq kuonyesha mshikamano wake na watu na serikali ya taifa hilo lililoghubikwa na vita.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja na waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abdi, amesema ana matumaini mji wa Mosul utakombolewa kabisa hivi karibuni na ameipongeza serikali kwa juhudi zake za kutaka

(Sauti ya Guterres CUT 1)

"Kuendelea kuunda mazingira ya kuwa na taifa la maisha ya kawaida , taifa ambalo jamii zote zitahisi hapo ni kwao, jamii zote zinaheshimiana na maridhiano kuwa kitu cha kawaida.”

Ameongeza kuwa Umoja wa mataifa unaunga mkono juhudi za serikali na utaendelea kuhakikisha misaada inawafikia walengwa walioathirika na machafuko katika sehemu mbalimbali za Iraq na akatoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa

(Sauti ya Guterres CUT 2)

"Kuisaidia Iraq katika suala la msaada kwa waathirika wa machafuko, lakini pia katika suala la kuleta utulivu na ujenzi mpya, na katika ujenzi wa taasisi za serikali za Iraq.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ziarani Iraq. Picha: UM
Amesema katika mazungumzo yake na waziri Mkuu al-Abdi wamegusia pia umuhimu wa suala la uwajibikaji kwa wanaotekeleza uasi hususani kundi la ISIL au Daesh

(Sauti ya Guterres CUT 3)

“Tumejadili jinsi ilivyo muhimu uhalifu uliotekelezwa na Daesh kuwajibishwa.Uhalifu huo unapaswa kufahamiaka , unapaswa kuadhibiwa na ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kufahamu kila kitu kilichofanyika, kuwatoa kafara watu wa Iraq wa aina zote Wasuni , Washia, Waislamu na Wakristo.”