Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa yaongeza madhila kwa watoto Somalia-UNICEF

Njaa yaongeza madhila kwa watoto Somalia-UNICEF

Amkani, si shwari tena Somalia! Ndivyo ilivyoanza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ikionya kuwa kuongezeka kwa njaa nchini Somalia kunaongeza idadi ya watoto ambao wanakabiliwa na utapiamlo na kipindu pindu. Flora Nducha na taarifa kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

UNICEF inasema kwamba watoto nchini humo wanakabiliwa na aina mbili za magonjwa yatokanayo na njaa ambayo ni unyafunzi na muunganiko wa kipindupindu na kuhara kutokanako na maji machafu magonjwa ambayo yaliua watoto wengi mwaka 2011.

Kwa mujibuwa UNICEF tangu mwanzo wa mwaka huu hadi kufikia Machi 28, kumeripotiwa visa zaidi ya 18,400 vya kipindupindu au kuharisha, huku mwaka jana ukishuhudia visa 15,600 hususani kwa watoto.

Shirika hilo la kuhudumia watoto limesema mwaka huu limeongeza mahitaji ya kifedha nchini Somalia, kutoka dola milini 66 hadi dola milioni 147, huku asilimia 54 ya kiwango hicho ikiwa haijatolewa na hivyo kutaka usaidizi zaidi.

Nalo Musdhaf ni miongoni mwa wakimbizi wa ndani nchini Somalia anayeishi kambini na watoto wake anaeleza mabadiliko.

( Sauti Nalo)

''Haikuwa hivi mwaka 2011, tulikuwa na maji yakitiririka katika mto. Lakini katika ukame huu, hakuna maji, na hakuna chakula kabisa. Hata kupata maji ya kunywa ni changamoto. Mwaka 2011 tuliuwa na maji visimani lakini sasa visima vimekauka.''