Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IRRI na FAO wasaidia kilimo endelevu cha mpunga

IRRI na FAO wasaidia kilimo endelevu cha mpunga

Shirika la chakula na kilimo FAO na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mpungu IRRI , wameafikiana kushirikiana kwa karibu zaidi kusaidia uzalishaji endelevu wa mpunga katika nchi zinazoendelea ili kuimarisha uhakika wa chakula na maisha ya watu huku wakilinda mali asili.

Muafaka uliiotiwa saini Alhamisi una lengo la kukusanya ujuzi wa kisayansi na teknolojia kutoka mashirika hayo mawili ili kuboresha na kupanua wigo wa kazi zao duniani.

La msingi katika ushirika huo ni kuimarisha mifumo ya kilimo endelevu cha mpunga kupitia shughuli za uwezeshaji ikiwemo utekelezaji wa mikakati na sera za kitaifa na kikanda ili kuwanufaisha wakulima wadogowadogo hususani wanawake.