Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubiš alaani vikali shambulio la kigaidi Yousufiyah Baghdad

Kubiš alaani vikali shambulio la kigaidi Yousufiyah Baghdad

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea Yousufiyah Baghdad nchini humo Jumatano jioni, ambapo watu kadhaa wameuawa au kujeruhiwa.

Bwana Kubiš amesema shambulio hilo la kinyama ni la pili kuilenga Baghdad chini ya siku kumi na limetekelezwa na magaidi wenye lengo la kulipiza kisasi kutokana na kushindwa kwenye mapambano mjini Mosoul na kwingineko.

Ameongeza kuwa mashambulio ya kinyama kama hayo hayatodhoofisha nia ya watu wa Iraq ambao wamejitolea kwa kila hali kuikomboa nchi yao kutoka kwa magaidi.

Ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.