Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwelekeo wa usajili wa watoto Tanzania una nuru- UNICEF

Mwelekeo wa usajili wa watoto Tanzania una nuru- UNICEF

Nchini Tanzania kampeni ya usajili watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano iliyoanza mwaka 2013, imesaidia kusogeza huduma za usajili karibu na jamii na hivyo kupunguza gharama zilizokuwa zinazuia baadhi ya wazazi kutotilia maanani mpango huo.

Kampeni hiyo inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali na wadau imewezesha wazazi kusajili watoto wao katika ofisi za kata badala ya kusafiri kati ya kilometa 80 hadi 100 hadi ofisi za wilayani.

Afisa mradi wa usajili vizazi UNICEF-Tanzania Baskhar Mishra ameiambia Idhaa hii kuwa kampeni hiyo pia imewezesha..

(Sauti ya Baskhar)

“Gharama ya usajili na cheti imeondolewa na serikali kwa ajili ya mradi huu, hivyo kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano, mfumo wa usajili haudai pesa yoyote ya usajili na cheti.”

 Tofauti na awali ambapo mzazi alipaswa kwenda zaidi ya mara moja wilayani ili kupata cheti hivi sasa..

 (Sauti ya Baskhar)

“Utoaji wa cheti unafanyika punde baada ya usajili na nakala ya kwanza ya cheti hupatiwa wazazi wa mtoto bila gharama yoyote.”

image
Aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba nchini Tanzania, Harrison Mwakyembe katika moja ya uzinduzi wa kampeni za usajili watoto, akiwa amembeba mmoja wa watoto waliosajliwa na cheti chake. (Picha:UNICEF-Tanzania)
Kampeni hiyo iliyoanza mwaka 2013, hadi sasa imefikia mikoa ya Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa, Njombe, Shinyanga na Geita ambapo watoto zaidi ya milioni moja wamesajiliwa.

Bwana Baskhar amesema mpango sasa ni kuongeza mikoa mingine sita ndani ya mwaka mmoja ujao na kushawishi serikali itengee bajeti mradi huo ili uwe endelevu.