Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa iamke dhidi ya uvunjifu wa haki- Bachelet

Jumuiya ya kimataifa iamke dhidi ya uvunjifu wa haki- Bachelet

Akilihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi hii leo, Rais wa Chile Michelle Bachelet amesema janga la watoto wakimbizi wa Syria na kuongezeka kuwa hotuba za chuki dhidi ya wageni lazima vikomeshwe kwa ushirikiano baina ya jumuiya ya kimataifa.

Bi Bachelet ambaye nchi yake inatetea kuteuliwa tena kuwa mwanachama wa bodi ya baraza hilo kwa mwaka 2018 amesema jumuiya ya kimataifa imesahau kuwa hotuba za chuki ndiyo chanzo cha mzozo wa Syria uliongia mwaka wa saba.

Hata hivyo amekiri kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu unaendelea, na kwamba baraza la haki za binadamu limekuwa legevu katika maeneo muhimu kama usawa, kukomesha ubaguzi wa utaifa, dini, jinsia, rangi au kabila.

Kwa upande wake Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema Chile imekuwa mtetezi wa siku nyingi wa haki za binadamu katika jukwaa la kimataifa lakini akaonya kuwa licha ya juhudi hizo za kukomesha utawala wa kiimla, familia nyingi bado hazifahamu ukweli kuhusu kilichotokea kwa wapendwa wao, hivyo akaonya.

( Sauti Zeid)

‘‘Haki ya kuelezwa ukweli wahanga wa ukiukwaji  wa ukatili wa haki za binadamu sio upendeleo, hatua zozote za msamaha au kuachiliwa mapema kwa watekelezaji wa uhalifu lazima kufanyike kwa umakini na kuzingatia haki za binadamu."