Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za kiarabu badilisheni mwelekeo ili msigeuzwe mtaji- Guterres

Nchi za kiarabu badilisheni mwelekeo ili msigeuzwe mtaji- Guterres

Umoja wa Mataifa umesihi viongozi wa nchi za kiarabu kuundwa kile ilichoita ulimwengu mpya wa kiarabu utakaowezesha nchi hizo kumaliza tofauti zao kwa njia ya mashauriano na mazungumzo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Ikiwa ni ziara yake ya pili huko Mashariki ya Kati ndani ya mwezi wa tatu wa uongozi wake wa Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema maelewano baina ya mataifa hayo ya kiarabu ni muhimu wakati huu ambapo baadhi ya nchi zimegeuza tofauti zao kuwa mtaji.

Akihutubia viongozi wa Umoja wa nchi hizo za kiarabu huko Jordan aliko ziarani Bwana Guterres amesema...

(Sauti ya Guterres)

Mgawanyiko ndani ya ulimwengu wa kiarabu umefungua milango kwa mataifa ya kigeni kuingilia kati kwa hadaa, kupanda mbegu ya ukosefu wa utulivu, mizozo ya kidini na ugaidi.”

Bwana Guterres akaenda mbali zaidi kuzungumzia vile ambavyo baadhi ya wanasiasa wanatumia dini ya kiislamu kujenga chuki dhidi ya madhehebu hayo na kutumbukiza ulimwenguni mikononi mwa vikundi vyenye misimamo mikali.

(Sauti ya Guterres)

“Watu wengi wametumbukia kwenye mtego wa vitendo vya aibu zaidi vya Daesh au Al Qaeda kana kwamba vinavyochochewa na uislamu, wakati ukweli ni kwamba wanachozungumza ni kinyume na imani ya dini ya kiislamu. Na wakati huo huo waislamu nao wanakuwa waathirika.”

Katibu Mkuu amesema wakati huu wa mizozo na majanga, umoja baina ya nchi za kiarabu ni muhimu kwa ajili ya ustawi na amani.