DRC inahitaji usaidizi zaidi bajeti sasa kuliko wakati mwingine: Balozi Mahiga
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhakikisha bajeti kwa ajili ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO inaongezwa ili kuhakikisha uimarishwaji wa amani katika ukanda huo.
Katika mhojiano na idhaa hii, saa kadhaa kabla ya kuhutubia kikao cha leo cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kinachoangazia hali nchini DRC, Balozi Mahiga anayemwakilisha mwenyekiti wa kitengo maalum cha amani na usalama cha nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara SADC, Rais John Magufuli wa Tanzania, anataja atakachokifanya nje ya kikao ili kushawishi kuongezwa kwa bajeti.
( Sauti Mahiga)

( Sauti Mahiga)