Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wengi wameuawa kwenye ukombozi Mosul: Zeid

Raia wengi wameuawa kwenye ukombozi Mosul: Zeid

Wito umetolewa hii leo kwa vikosi vya ulinzi na usalama nchini Iraq kuchukua "tahadhari kubwa"iwezekanavyo katika kampeni zao za kuikomboa Mosul kutoka kwa wanamgambo ISIL huku kukiwa na taarifa kwamba mamia ya raia wameuawa katika mashambulizi ya anga.

Ombi hilo limetolewa na ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa baada ya mashahidi kuelezea kuwa waasi wenye msimamo mkali waliwalilazimisha kukaa katika nyumba zao wakishambuliana na majeshi ya serikali.

Kamishna Mkuu Zeid Ra’ad Al-Hussein amekaribisha tangazo la vikosi vya majeshi ya muungano wa kimataifa kwa kufanya uchunguzi dhidi baadhi ya matukio hayo makubwa yaliyofanywa dhidi ya raia.

Msemaji  wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, uswis hii leo kwamba kwenye mapigano ya kuikomboa Mosul, makombora yaliyorushwa yalisababisha majeruhi na pia kuua raia.

Akiongeza kwamba suala hilo ni ngumu kutokana na ukweli kwamba ISIL, au Daesh, kwa makusudi walihifadhi mabomu kwenye majengo ya raia na kwamba...

(Sauti ya Rupert)

"Shahidi baada ya shahidi wametuambia kwamba ISIL iliwalazimisha kubaki ndani ya nyumba zao, na hata kuwafungia ndani, wakati wapiganaji hao walikaa juu ya paa ili kufanya mashambulizi dhidi ya jeshi la Iraq. Mashahidi vile vile wametuambia kuwa ISIL iliwaarifu kwamba ni jambo bora kufa kwa ajili ya nchi yao. Hii inaeleza kwa nini waliwalenga kwa makusudi raia waliojaribu kukimbia”.

Taarifa hiyo imesema kuwa tukio baya zaidi katika kampeni ya kuikomboa Mosul mnamo Machi 17 liliwaua karibu watu 60. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, zaidi ya watu 307 wameuawa kati ya Februari 17 na Machi 22.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba karibu watu 280,000 wameyakimbia makazi yao tangu kuanza kwa operesheni ya Mosul Oktoba mwaka jana.