Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vimbunga Matthew na Otto vyastaafishwa: WMO

Vimbunga Matthew na Otto vyastaafishwa: WMO

Ni kawadia kusikia watu wakistaafu baada ya kufuikia umri fulani kwa mujibu wa sheria za nchi!

Hii imekuwa tofauti kwa binadamu, vimbunga Mathew na Otto ambavyo vimesababisha madhara makubwa yakiwemo vifo na uharibifu wa mali na pia madhara ya kiafya, vimestaafishwa rasmi leo na shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO.

Majina ya vimbunga hivyo yamestaafishwa rasmi leo baada ya kusababisha majanga makubwa kwa mwaka 2016  Martin inachukua nafasi ya Mathew na Owen badala ya Otto. Huu ni utaratibu wa shirika hilo wa kutoa majina kwa vimbunga.

WMO katika taarifa yake hiyo ya kustaafisha visababishi hivyo vya majanga imesema uamuzi huo umefikiwa wakati wa mkutano wa kamati za kanda za Carribia, Ghuba ya Mexico, Kaskazini mwa bahari ya Atlantic , Mashariki na Kaskazini mwa bahaari ya Pasific

Mkutano uliofikia uamuzi huo umefanyika nchini Costa Rica, ambapo tathimini ya vimbunga kwa mwaka 2016 iliyojikita katika kuimarisha huduma za maandalizi ya onyo dhidi ya majanga hayo katika ukanda huo katika siku zijazo