Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC, Kenya wazindua muongozo wa kukabalina na ugaidi.

UNODC, Kenya wazindua muongozo wa kukabalina na ugaidi.

Ikiwezeshwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC, serikali ya Kenya kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, leo wamezindua muongozo wa kuzingatia haki za binadamu na kushugulikia uhalifu wa kigaidi nchini humo.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kukabliana na ugaidi duniani, unaosisitiza jukumu muhimu la kuheshimu haki za binadamu na utawala wa kisheria ikiwamo kulinda haki za wahanga wa ugaidi.

Muongozo huo utatumika kama mafunzo na kifaa rejea kwa wapelelezi, waendesha mashtaka na maafisa wa mahakama amesema Dorcas Oduor ambaye ni mwendesha mashataka wa serikali wa Kenya wakati wa uzinduzi huo leo.

Ameongeza kwamba muongozo huo utapigia chepuo uelewa wa hatariya ugaidi na umuhimu wa kuzingatia utawala wa kisheria hususani kwa haki za msingi za washukiwa.

Kwa upande wake mwakilishi wa UNODC ukanda wa Afrika Mashariki José Vila del Castillo, amesema uzuiaji wa uhalifu na ugaidi na mikakati ya haki kwa wahalifu lazima vitekelezwe kwa misingi ya haki za binadamu.

Muongozo huo unaainisha masuala ya haki za binadamu yanayojitokeza wakati wa uchunguzi, kesi na adhabu kwa makosa ya kigaidi katika mukatdha wa sheria za Kenya na za kimataifa, hasa kwa kuzingatia kwamba wadau hao wamekuwa wakikabiliwa na hoja ngumu ambazo zimejumuishwa kwenye muongozo.