Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto za wananchi wa Sudan Kusini kuwa taifa lao huru litaimarika

Ndoto za wananchi wa Sudan Kusini kuwa taifa lao huru litaimarika

Kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa Machi, Mwenyekiti mpya wa kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU Moussa Faki Mahamat alikuwa ziarani nchini Sudan Kusini kujionea hali halisi wakati huu ambapo janga la kibinamu linazidi kupanuka, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu tangu mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uibuke nchini humo. Ndoto za wananchi kuwa taifa lao huru litaimarika na kuchanua, zimetumbukia nyongo huku mapigano yakishika kasikila uchao na watoa misaada nao wakiwindwa. Je nini amejionea Bwana Mahamat, katika ziara yake ya kwanza tangu achaguliwe kuongoza kamisheni ya AU? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.