Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaalani vikali mauaji ya polisi 40 wa serikali DRC: UM/AU/EU

Tunaalani vikali mauaji ya polisi 40 wa serikali DRC: UM/AU/EU

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Africa, AU pamoja na Muungano wa Ulaya, EU wamelaani vikali ripoti za mauaji ya polisi 40 wa serikali yaliyotekelezwa na waasi wa Kamuina Nsapu katika wilaya ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mwezi Machi. Taarifa kamili na Rosemary Musumba

(TAARIFA YA ROSEMARY)

Mauaji hayo yaliyofanyika katikati mwa barabara za Tshikapa na Kananga ni moja ya matukio ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wilayani humo, yamesema mashirika hayo, na kutoa wito kwa serikali kutafuta suluhisho la amani la haraka.

Hivyo katika jitihada za kurejesha utulivu na amani Kasai, wamevisihi vikosi vya ulinzi na usalama kujizuia na matumizi ya nguvu, na kuihimiza serikali kuendeleza mazungumzo na wanamgambo wa Kamuina Nsapu.

Pia yametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, na kusisitiza haja ya uchunguzi na uwajibishaji wa wahusika wa tukio hilo.