Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Surua yashambulia kwa kasi Ulaya: WHO

Surua yashambulia kwa kasi Ulaya: WHO

Kama ulifikiri surua inashambulia bara Afrika pekee, lahasha! Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya visa 500 vimeripotiwa barani Ulaya ifikapo jana Januari 27 huku ugonjwa huo unaoathiri watoto ukidaiwa huenda ukisasabisha mlipuko mkubwa zaidi kutokana na kupungua kwa chanjo kwa asilimia 95.

WHO inasema katika taarifa yake ya leo kwamba kwa kipindi cha miaka miwili kiwango cha surua kimeongezeka barani humo na kuongeza kuwa ikiwa kiwangco stahiki cha chanjo hakitafikiwa, ugonjwa huo utaendelea barani Ulaya na kwingineko.

Mkuu wa WHO ukanda wa Ulaya Zsuzsanna Jakab,amenukuliwa katiak taarifa hiyo akisema kuwa muundo wa sasa wa kusafiri haumuweki mtu salama dhidi ya surua.

Nchi ambazo zimetajwa na shirika la afya ulimwenguni kuwa na kiwango kikubwa cha surua barani Ulaya ni Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland Romania, Uswisi na Ukraine.