Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Milio ya risasi na mabomu yaendelea kunguruma Yemen licha ya juhudi za kimataifa

Milio ya risasi na mabomu yaendelea kunguruma Yemen licha ya juhudi za kimataifa

Licha ya juhudi za kimataifa za kuleta suluhu ya kudumu ya kisasa Yemen, milio ya makombora, mabomu, risasi na vifaru sasa imekuwa ada katika maisha ya kila siku nchini humo. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Hayo yamesemwa na Stephen O’Brien msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, katika taarifa yake kuhusu miaka miwili baada ya kuzuka machafuko Yemen.

Amesema maelfu ya raia wameuawa, wakiwemo wasichana na wavulana zaidi ya 1400, wengi wa watoto hao walitoka majumbani kwao kuelekea shuleni na hawakurejea tena, huku raia wengine kwa maelfu wakijeruhiwa.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema hali ngumu nchini Yemen imesababisha familia kugeukia mbinu hatari kukidhi mahitaji.

Dkt. Sherin Varkey, ni Naibu Mwakilishi wa UNICEF nchini Yemen...

(sauti ya Sherin)

“Tuna wasiwasi zaidi kwa kuwa kutokana na kutokulipwa kwa mishahara kwa muda mrefu sasa na kutokana na kutokuwepo kwa kipato, familia nyingi zinakosa uwezo wa manunuzi na uwezo wao wa kununua chakula na kulea watoto wao.”